DAR ES SALAAM-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imempa kandarasi ya miaka miwili mlinda mlango, Jefferson Luis Szerban (29) raia wa Brazil.
Simba SC wamemsajili Jefferson kutoka klabu ya Resende FC ya Brazil ambapo msimu uliopita aliichezea Itabirito FC-MG kwa mkopo.
Tayari mlinda mlango huyo ameungana na kikosi nchini Uturuki kuendelea na mazoezi ya maandalizi ya msimu wa mashindano 2023/24 akitokea Brazil.
Kwa mujibu wa uongozi wa Simba SC, Jefferson ana uwezo mkubwa wa kulinda lango huku akitumia miguu yote kwa ufasaha pamoja na kumudu kuanzisha mashambulizi.
Jefferson ambaye ana urefu wa futi 1.92 amekuja kuungana na walinda milango, Aishi Manula, Ally Salim na Ahmed Feruzi ‘Teru’.
Pia, Jefferson ana uzoefu wa kucheza mechi nyingi za ushindani, hivyo Simba SC wanaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu hasa ukizingatia Manula atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu.