DAR ES SALAAM-Uongozi wa Simba SC umefikia makubaliano na Klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa kumnunua mchezaji wao Pape Ousmane Sakho.
Picha na Goal.
"Simba SC tumefikia makubaliano na klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa kumnunua mchezaji wetu Pape Sakho.Tunamtakia kila la kheri Sakho kwenye timu yake mpya,"imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Simba SC.
Sakho ambaye ni mzaliwa wa Rufisque huko nchini Senegal kwa sasa akiwa na umri wa miaka 26 alijiunga na Wekundu wa Msimbazi tarehe 14 Agosti, 2021 akitokea Teungueth FC ya Senegal.
Aidha,baada ya misimu miwili mizuri anaondoka Simba SC ikiwa kandarasi yake ilipaswa kufikia tamati Juni 30, 2024.