MISRI-Hatimaye michuano ya soka barani Afrika imewadia ambapo Mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, Tanzania Bara inawakilishwa na klabu za Yanga na Simba wakati kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho, Tanzania Bara itawakilishwa na Azam FC na Singida Fountain Gate FC.
Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu ulioisha, Yanga SC wataanza raundi ya awali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa, wakicheza dhidi ya ASAS ya Djibouti huku wakisubiri mshindi wa jumla kati ya Association Sportive Otohô ya Congo au El Merreikh ya Sudan ili kucheza nao kwenye raundi ya kwanza.
Simba SC wao wataanza raundi ya kwanza ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika wakisubiri mshindi wa jumla kati ya Africans Stars ya Namibia au Power Dynamos FC ya Zambia.
Aidha, Azam FC watacheza dhidi ya Bahir Dar Kenema FC ya Ethiopia, kwenye raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika, mshindi wa jumla katika mchezo huo atakutana na Club Africain ya Tunisia kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
Singida Fountain Gate FC wataanza raundi ya JKU SC ambapo mshindi wa jumla atacheza dhidi ya Future FC ya Misri kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
Droo hiyo ya CAF imepangwa Julai 25, 2023 na mechi hizo za awali zitachezwa kati ya Agosti 18, 19, na 20 huku mechi za marudiano ni kati ya Agosti 25, 26 na 27, 2023.

Tags
Habari
Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika
Kombe la Shirikisho Afrika
Michezo
Simba SC
Yanga SC