KILIMANJARO-Klabu ya Simba SC imefanikiwa kuzindua jezi zao ambazo watazitumia kwenye mashindano mbalimbali msimu ujao kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Kwenye jezi hizo, wameandika majina mgongoni ya viongozi wa wakuu wa Serikali ikiwa ni kuthamini mchango wao.
Jezi hizo ambazo zimezinduliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro zina majina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa.
Nyingine ni majina ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Tulia Akson na Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’.
Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula aliweka wazi kuwa baada ya jezi hizo kushuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro zitapigwa mnada na pesa zitakazopatikana zitajenga wodi ya wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Taifa Zanzibar.
Kajula amesema, kile kibegi kilichotumika kubebeza jezi hizo kitapelekwa Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vijavyo kutokana na umaarufu kilichojizolea.