NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma amefungua na kufunga mbio za masafa marefu za Kiswahili (Swahili Marathon) zilizofanyika jijini Arusha ikiwa ni kuelekea Kilele cha Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7, 2023.
Mhe. Mwinjuma ameongeza kuwa mbio hizo zinalenga kuchochea na kuendeleza juhudi za kutangaza utalii wa Tanzania ambazo zilianzishwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania kupitia filamu aliyoianzisha ya Royal Tour.