DAR ES SALAAM-Habari za muda huu ndugu Watanzania, dada (pichani) anaitwa Adivela au Anne ni mzaliwa wa Ukerewe katika Kijiji cha Nyakaturu mkoani Mwanza,tarehe 12 Jumatano usiku wa kuamkia tarehe 13,2023 amefariki kwa tatizo la kuishiwa damu (Sickle cell).
Amefia ndani alipokuwa amelala na wafanyakazi wenzake katika Bar za Mzee Mirambo Buguruni kwa Mnyamani alipokuwa akifanya kazi.
Mpaka sasa mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam na wamepewa siku tisa tu za mwili kuhifadhiwa.
Kwa anayemfahamu tafadhali share taarifa hii ili ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki.
Kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kuzungumza na mtu aliyekuwa na marehemu enzi za uhai wake simu 0672 089 440.