TEF:Shambulio lolote kwa wanahabari halikubaliki

DAR ES SALAAM-Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani kitendo cha waandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Sunday George, Fortune Francis na dereva wao Omary Mhando kushambuliwa na vijana wakati wakitekeleza majukumu yao.

Hayo yamebainishwa kupitia tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa TEF,Deodatius Balile na kufafanua kuwa, shambulizi hilo lilitokea Julai 22, 2023 katika Uwanja wa Bulyaga uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Ni wakati, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiwa katika maandalizi ya mkutano wake wa hadhara.

"Kundi la vijana kwenye viwanja hivyo, liliwavamia waandishi hao pamoja na dereva na kuwashambulia kisha kufanya uharibifu mkubwa wa gari walilokuwa wanatumia kwa kuvunja kioo cha nyuma pamoja na kuwaibia simu zao.

"Taarifa za tukio hilo zimeripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang'ombe, Temeke jijini Dar es Salaam. Shambulio lolote kwa waandishi wa habari halikubaliki.

"Kitendo kilichofanywa na vijana hao ni cha kulaaniwa kwa kuwa, kinadhalilisha na kurudisha nyuma juhudi za tasnia ya habari.

"Kutokana na tukio hilo, Jukwaa la Wahariri linatoa pole kwa wanahabari w aliofikwa na tukio hilo akiwemo dereva, lakini pia kwa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd.

"Jukwaa la Wahariri Tanzania tunakumbusha vyama vya siasa kutuliza mihemko ya wanachama wao pale wapotaka ama kupanga mashambulizi dhidi ya wanahabari."

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news