DAR ES SALAAM- Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwepo wa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa.
Sambamba na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili yatakayodumu kwa siku tano kuanzia Julai 27,2023 ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamala hiyo Julai 26,2023.
TMA imetaja baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi yatakayokabiliwa na hali hiyo kuwa ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani, ikijumuisha visiwa vya Mafia pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Maeneo mengine ni ya Ukanda wa Ziwa Victoria ambayo yanajumuisha mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara pamoja na ukanda wa Ziwa Nyasa, mikoa ya Mbeya, Njombe na Ruvuma.
TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza ambazo ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafirishaji baharini.