Tunzeni vifaa vya michezo

NA ADELADIUS MAKWEGA 

MKUU wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, Mkufunzi Richard Mganga amewataka wanamichezo wote nchini, kujenga tabia ya kutunza vifaa vya michezo, popote walipo, maana kinyume chake yatafanyika matumizii makubwa ya ununuzi wa vifaa hivyo kila mara, kumbe fedha hizo zingetumika kwa matumizi mengine. 
Hayo yamesemwa na mkufunzi Mganga wakati akizungumza na Serikali ya Wanachuo ya Chuo hicho mapema Julai 6, 2023 wakati wakifanya kikao cha utambulisho wa serikali yao mpya mara baada ya kuchaguliwa na kula kiapo, hivi karibu.

“Ninachofahamu katika shule zetu nyingi, wanafunzi wakishacheza michezo wanasema kila mmoja atafua jezi yake, hivyo wanarudi nazo nyumbani.
"Siku inayofuata ukimualiza jezi ipo wapi? Majibu yake, jezi imepotea, hivyo kwenu nyinyi ambao mnasomea kufundisha michezo mnatakiwa kuwa makini na utunzaji wa vifaa vya michezo kila mara ili somo hili liweze kuwafikia wananamichezo wote wa taifa letu au popote mlipo.” 

Akiendelea kutoa maelekezo yake kwa uongozi mpya, mkufunzi Mganga alisema kuwa zipo changamoto kadhaa chuoni hapo lakini Serikali inaendelea kuzifanyia kazi, kama alivyoeleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ndugu Said Yakubu , hivi karibuni alipotembelea taasisi hii.
Awali mkufunzi Mganga alipokea ugeni wa vijana kutoka Ufaransa na Ujerumani ambao walitembelea chuo hicho , huku kwa siku mbili walishiriki michezo kadhaa na kutoa zawadi ya vifaa vya michezo kama vile jezi na mipira ya michezo mbalimbali. 

Akizungumza kando ya shughuli hizo Makamu Mkuu wa Chuo hicho, mkufunzi Alex Mkenyenge amesema kuwa anawashukuru wageni hao kufika Malya na anawakaribisha tena na tena. Kwa viongozi wa serikali ya wanachuo , mkufunzi Mkenyenge amesema, 
“Anawaomba wasome kwa bidii maana itakuwa aibu kwa kiongozi wanachuo kufeli mitihani hiyo au kila mara akionekana anafanya mitihani ya marudio.” 

Kwa ujumla kwa sasa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kinaendelea na muhula wa mwisho wa mwaka wa masomo wa 2022/ 2023 huku mitihani ya majaribio ikifanyika na baada ya hapo itafanyika mitihani ya mwisho wa mwaka, huku juma lijalo mahafali ya vikundi vya dini kwa wanachuo yakitarajiwa kuanza kufanyika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news