Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akipewa maua ya pongezi na Mtumishi wa Wizara hiyo, Bi. Lucylily Mlay, alipowasili katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam, baada ya kuapishwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuiongoza Wizara hiyo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa nne kushoto), Manaibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Jenifa Omolo (wan ne kulia) na Bw. Elijah Mwandumbya (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Idara na Vitengo vya Wizara hiyo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Mhe. Nathan Belete (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja walipowasili katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam, baada ya viongozi wa Wizara hiyo kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano WFM, Dar es Salaam).