DAR ES SALAAM-Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema vyama vipya vya siasa 18 vimeomba usajili ambapo utaanza kutekelezwa baada ya kuhitimishwa zoezi la uhakiki wa vyama vilivyopo.

Mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kwenye uhakiki ambapo amesema hawezi kusajili vyama vipya kabla ya kufanyika uhakiki kwa vyama vilivyopo. Uhakiki wa vyama unatarajiwa kufanyika Julai 20, mwaka huu.
Amesema, wanaotaka kufuta hati chafu ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa kuhakikisha vyama vinakuwa na wataalamu wa fedha ambao watakuwa wanafanya shughuli kwa kuzingatia weledi.