ADDIS BABA-Waziri Mkuu wa Ethiopia,Dkt.Abiy Ahmed amemteua, Bi.Teyiba Hassen kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa kike kuongoza Idara ya Huduma ya Wakimbizi na Waliorejea nchini humo (Refugees and Returnees Service (RRS).
Kabla ya kazi hii, Bi.Teyiba amekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa RRS.Teyiba anatajwa kuwa miongoni mwa wanawake wenye uzoefu wa kufanya kazi katika mazingira magumu, ikiwemo kuongoza operesheni ya wakimbizi nchini Ethiopia.
Pia, kwa sasa ana jukumu la kuzidisha juhudi za kusimamia mwitikio tata wa wakimbizi nchini Ethiopia.
Pia, kwa sasa ana jukumu la kuzidisha juhudi za kusimamia mwitikio tata wa wakimbizi nchini Ethiopia.
Teyiba anachukua nafasi ya juu wakati Ethiopia inawakaribisha zaidi ya wakimbizi milioni moja na wanaotafuta hifadhi licha ya kupungua kwa misaada ya kibinadamu na maendeleo kutoka kwa jumuiya za kimataifa, wafadhili na washirika wake.
Aidha, Pembe ya Afrika likiwa eneo lenye hali tete, litakuwa mojawapo ya majukumu ya Teyiba ambaye pia ni mshauri wa masuala ya Kijamii wa Waziri Mkuu, Abiy Ahmed.
Wakati huo huo, Bi.Teyiba ametangazwa kuwa Meya wa mji wa Shashemene na Naibu Rais wa Jimbo la Oromia ambalo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018 lina wakazi zaidi ya milioni 35 huku likiwa na ukubwa kilomita za mraba 353,690.