Waziri Mkuu:Nendeni mkakope ili mpate vifaa vya kisasa na kupata tija kupitia kilimo

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema thamani ya mikopo inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeongezeka kutoka shilingi milioni 776 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 317 mwezi Juni, mwaka 2023 huku akiwataka wananchi kwenda kukopa waweze kupata tija katika shughuli za kilimo.
Mheshimiwa Majaliwa amesema mafanikio makubwa ni azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwainua wakulima wa Tanzania na kuendeleza Sekta ya Kilimo kwa ujumla.

Amesema hayo leo Julai 6, 2023 wakati alipozindua Ofisi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania katika Kanda ya Kusini, Mtwara.
“Ukuaji huo umechagizwa na ongezeko la mtaji kutoka shilingi bilioni 61.09 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 302.01 katika mwaka 2022.
Ninawapongeza sana kwa hatua hiyo kwani kadri mtaji unavyoongezeka na uwezo wa kuhudumia wakulima kwa njia ya mikopo unaongezeka.”

Akizungumza baada ya uzinduzi wa Ofisi hizo Mheshimiwa Majaliwa amewataka wananchi wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kuchangamkia fursa ya uwepo wa Ofisi hiyo ya Kanda Mtwara kupata uelewa zaidi kuhusu utaratibu wa kupata mikopo. “Nendeni mkakope ili mpate vifaa vya kisasa na kupata tija kupitia kilimo.”
“Menejimenti ya Benki na watumishi wa Ofisi ya Kanda ya Kusini wekeni masharti nafuu katika kutoa mikopo ili kuwezesha mikopo kwa wakulima, wavuvi na wafugaji kwa wakati.”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imetenga shilingi bilioni 35 kwa ajili ya mpango wa kuwakopesha wakulima wa korosho ili kuendeleza zao hili. 

“Ni matumaini yangu kwamba fedha hizi na nyingine ambazo mtaendelea kuwekeza huko zitajikita katika kufanikisha malengo”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news