Waziri Nape alaani wanahabari kushambuliwa Dar

DAR ES SALAAM-Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mheshimiwa Nape Nnauye amelaani tukio la waandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na dereva wa kampuni hiyo kushambuliwa, kijeruhiwa kwa kupigwa na kundi la vijana ambao hawajafahamika wa chama gani.
Kwa mujibu wa Mwananchi, tukio hilo lilitokea mchana wa Julai 22, 2023 wakati waandishi na dereva walipofika kufuatilia maandalizi ya mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) unaotarajia kufanyika leo Jumapili Julai 23,2023.

Aidha, mbali na kujeruhiwa kwa waandishi hao na dereva, pia wameibiwa simu za mkononi pamoja na gari kuharibiwa kwa kuvunjwa vioo.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Mheshimiwa Waziri Nape ameandika ujumbe wa kulaani tukio hilo akiambatanisha na picha ya gari lilivyoharibiwa na vijana hao.

"Nimestushwa na kitendo hichi. Nalaani utamaduni wa kuwashambulia waandishi wakati wakitimiza majukumu yao.Naamini vyombo vitachukua hatua zinazostahili, kwani sidhani kama ni ngumu kuwapata waliofanya tukio hili kwasababu eneo na kazi walizokwenda kufanya Waandishi zinajulikana."

Hata hivyo, kwa mujibu wa Mwananchi tayari uongozi wa MCL umeripoti tukio hilo Kituo cha Polisi cha Chang’ombe kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini kama hatua ya awali wakati taratibu zingine za kiofisi zikiendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news