Waziri Simbachawene atoa rai nchi za Afrika kuhusu rushwa

NA LUSUNGU HELELA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema rushwa Barani Afrika ni tatizo linalohitaji njia ya pamoja ya kupambana nalo kwani utoaji na upokeaji rushwa unabadilika kulingana na msukumo wa maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja maisha ya watu kadiri yanavyobadilika. 
Imeelezwa kuwa ni muda muafaka sasa kwa nchi za Afrika kuwa na sheria zinazofanana katika kushughulikia tatizo hilo, hali itakayopelekea kutokomeza kabisa tatizo la rushwa. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa, ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha, Mhe. Simbachwene amesema mbinu za kupambana na rushwa ni lazima kubadilika kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. 
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano hilo ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Amesema kongamano hilo ikiwezekana litoke na maazimio ya pamoja yatakayopelekea nchi zote za Afrika kuwa na sheria zinazofanana ili watuhumiwa wa rushwa wa nchi hizo wajue kabisa kuwa watawajibishwa kupitia sheria hizo. 
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano hilo ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Amesema kuwa tatizo la rushwa Barani Afrika ni kubwa na linahitaji sauti ya pamoja huku akitolea mfano wa rushwa kwenye suala la utoaji wa elimu na kusema kuwa kama hatua za pamoja hazitachukuliwa kutapelekea kuwa na vijana wahitimu ambao ni zao la rushwa. 
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano hilo ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Kufuatia hatua hiyo amezihimiza nchi za Afrika kutumia Kongamano hilo kujadili namna bora ya kutumia sayansi na teknolojia katika utoaji huduma utakaowezesha kuzuia watu kukutana ana kwa ana huku akisisitiza mifumo hiyo iwekwe ili kudhibiti rushwa katika sekta mbalimbali. 
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) CP. Salum Hamduni amesema Kongamano hilo, mbali ya kuwakutanisha Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika pia limewakutanisha Wadau wa kupambana na rushwa wa ndani na nje ya nchi, hivyo Kongamano hilo ni darasa huru la kujifunza na kupata uzoefu wa kupambana na rushwa kwa nchi moja moja na Afrika kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa rushwa inatokomezwa kabisa. 

Ameongeza kuwa Kongamano hilo pamoja na kujadili mada mbalimbali za kupambana na rushwa Barani Afrika pia watajadili mbinu mbalimbali za kupambana na tatizo hilo kidigitali ikizingatiwa kuwa utoaji wa rushwa kwa sasa unafanyika kidigitali. 
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la kujadili namna bora ya kupambana na rushwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano hilo ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika ambayo hufanyika kila mwaka Julai 11, na mwaka huu 2023 maadhimisho hayo yanafanyika hapa Tanzania, jijini Arusha.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufikia tamati Julai 11, 2023 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news