Waziri Ummy awakaribisha Nephroplus kuwekeza nchini kupunguza gharama za kusafisha damu

HYDERABAD-Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ameukaribisha uongozi wa Taasisi Nephroplus ya nchini India kuja kuwekeza nchini ili kusaidia kupunguza gharama za kusafisha damu.
Waziri Ummy amesema hayo wakati akihitimisha ziara yake nchini India kwa kutembelea Taasisi ya Nephroplus.

Waziri Ummy amesema, Tanzania ina uhitaji mkubwa wa huduma za kuchuja damu ndio sababu ya Serikali imeamua kutafuta wadau wa kushirikiana nao kuwezesha kupunguza gharama ili kuwafikia watanzania wengi wenye uhitaji hasa kwa watu wasio na bima ya afya.

"Serikali iko tayari kuingia makubaliano ya ushirikiano na taasisi hii kwa kuwa mapendekezo ya gharama zao ni za chini na hivyo kila mwananchi mwenye uhitaji ataweza kumudu gharama za huduma hiyo muhimu,"amesema Waziri Ummy.
Ameongeza kuwa, uwekezaji huo utasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo kwa gharama nafuu nchini.

Taasisi ya Nephroplus iliyopo mjini Hyderabad nchini India inajishughulisha na utoaji wa huduma za kuchuja damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo imedhamiria kuwekeza katika huduma za upatikanaji wa huduma za kuchuja damu nchini. 
Taasisi hiyo ina jumla ya vituo vya kusafisha damu takribani 325 katika miji 20 nchini India na nje ya India. Aidha, taasisi hiyo ina jumla ya mashine za kusafishia damu zipatazo 4,500. 

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi hiyo,Vikram Vupalla ameeleza kuwa, wamekuwa na mafanikio makubwa kwenye nchi wanazotoa huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo. 
Pia, ameeleza nia yake ya kuja kuwekeza na kutoa huduma za kusafisha damu nchini kwa gharama nafuu.

Vupall amesema kuwa, ili aweze kuwekeza nchini anahitaji ushirikiano wa Wizara ya Afya na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha uwekezaji huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news