Yanga SC yapewa heshima nchini Malawi

NA DIRAMAKINI

MABINGWA wa soka nchini Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imepewa mwaliko maalumu na Serikali ya Jamhuri ya Malawi kuelekea maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Taifa hilo la Kusini mwa Afrika.

"Tumepokea mwaliko maalumu kutoka kwa Serikali ya Malawi kucheza mchezo maalumu kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi itakayofanyika Julai 6, 2023. Ni heshima kubwa sana kwa Klabu yetu na kwa Taifa kwa ujumla;

Hayo yamebainishwa Julai 3, 2023 na Afisa Habari Young Africans SC, Ally Kamwe wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

"Mgeni wa heshima kwenye sikukuu za uhuru wa Malawi ni Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali ya Malawi ikatupa heshima hii ya kipekee kwa mualiko huu mkubwa na wa kihistoria.

"Napenda kutoa shukrani na pongezi kwa wachezaji wetu ambao watatoka mapumzikoni na kuungana nasi kwenda kuiwakilisha nchi na klabu yetu kwenye mualiko huu mkubwa.

"Tunatarajia kuondoka siku ya Jumatano na kama kawaida yetu ndege maalum kabisa itatupeleka Malawi na kutusubiri kisha tutarejea Dar es Salaam siku ya Alhamisi baada ya sherehe hizo,"amefafanua Afisa Habari huyo.

Katika hatua nyingine,Afisa Habari Young Africans SC, Ally Kamwe amesema,"Thank you bado hazijafika mwisho, bado zinaendelea, wapo wachezaji na baadhi ya watendaji kwenye idara mbalimbali ambao ndani ya wiki hii watapewa thank you na kuwafungulia fursa wakapate changamoto kwenye maeneo mengine.

"Mpaka sasa hivi tumemaliza usajili kwa msimu huu, wachezaji wote ambao tulikuwa tunawahitaji tayari wameshasaini, tumefunga zoezi la usajili kinachofuatia ni kuwatambulisha wachezaji hawa na zoezi hilo litaanza baada ya utambulisho wa jezi mpya,"amefafanua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news