Zingatieni matumizi sahihi ya fedha za maendeleo-Dkt.Mabula

NA MUNIR SHEMWETA

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ameagiza kuwepo usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akisalimiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Jimbo la Ilemela.

Dkt.Mabula ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela amesema hayo Julai 4, 2023 jijini Mwanza akiwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.

Katika ukaguzi huo, Waziri Dkt.Mabula alisisitiza pia umuhimu wa matumizi thabiti ya fedha za maendeleo sambamba na uzalendo wakati wa katika utekelezaji wa miradi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akikagua miradi ya maendeleo katika Jimbo la Ilemela Mkoa wa Mwanza.

"Ni viźuri wakati wa utekelezaji miradi katika Jimbo la Ilemela mkahakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya fedha za maendeleo, lakini pia uzalendo uwekwe mbele,"amesema Dkt.Mabula.

Waziri huyo wa Ardhi na Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza alifanya ukaguzi wa miradi katika Kata ya Bugogwa, Shule ya Msingi Igombe ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi Milioni 69, 100,000 kupitia mradi wa Boost kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa Shuleni hapo .
Lakini pia amefanya ukaguzi kata ya Kahama katika ujenzi wa Shule mpya ya Msingi inayojengwa kata ya Kahama ambapo serikali imetoa zaidi shilingi Milioni 540 ,300,000. kupitia mradi wa Boost pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Buswelu - Busenga ambapo serikali pia imetoa zaidi tsh Milioni 540,300,000. kufanikisha ujenzi wa Shule hiyo .

Aidha, alifanya ukaguzi wa ujenzi wa Bweni la watoto wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Buswelu ambapo Serikali imetoa zaidi ya Milioni 100 kufanikisha ujenzi wa Bweni hilo na zahanati mpya iliyojengwa kata ya Ilemela mtaa wa Lumala ambapo zaidi ya shilingi milioni 142 zimetumika kujenga zahanati hiyo ambapo pia Mhe Mbunge amechangia tofali zaidi 3500. 
Moja ya mradi unaotekelezwa katika jimbo la Ilemela mkoa wa Mwanza.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi uliofanywa na Dkt.Mabula katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Ilemela, Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Hassan Milanga alimpongeza Mbunge wa jimbo hilo kwa uchapakazi wake ambapo alibainisha kuwa chama cha Mapinduzi wilayani humo kinatambua jitihada zake katika kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Ilemela 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Hassan Masala alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuipatia Ilemela fedha nyingi za miradi na kueleza kuwa fedha hizo zinakwenda kutatua changamoto mbalimbali katika Wilaya ya Ilemela

Akihitimisha ziara hiyo, Waziri Mabula alitoa wito Kwa wananchi kuendelea kumuunga mkono Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kazi kubwa ya maendeleo anayoifanya jimboni Ilemela 

Aliwashukuru wananchi wa kata ya Ilemela Kwa kuendelea kuiamini serikali lakini pia Kwa ushirikiano wanaoutoa Kwa serikali .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news