KILIMANJARO-Watu 10 wamefariki dunia akiwemo askari polisi na mmoja kujeruhiwa baada ya gari la polisi kugongana na gari dogo la mizigo maarufu kama Kirikuu katika eneo la Datch kona wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kuwa, ajali hiyo imetokea Agosti 18,2023, ambapo wananchi tisa walikuwa kwenye gari la Kirikuu wakielekea katika mnada wa mifugo wa Ngarenairobi wilayani humo.
Alisema kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni gari la Kirikuu kupasuka tairi na kukosa mwelekeo na kugongana na lori la polisi ambapo nalo lilikosa mwelekeo na kugonga mti.
“Kutokana na tukio hilo watu kumi wamefariki dunia pale pale, kati ya hao tisa walikuwa kwenye gari ya kirikuu na dareva wake pamoja na dereva wa lori la polisi ambaye ni askari polisi,”alisema Babu.
Alisema kuwa, waliofariki katika ajali hiyo ni wanawake sita pamoja na wanaume wanne akiwemo askari wa Jeshi la Polisi.
Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi kutambua kuwa magari aina ya kirikuu, pikapu na malori sio magari ya kubeba abiria bali ni magari ya mizigo, hivyo ni marufuku wananchi kupakia magari hayo kama magari ya abiria.