Akiba ya fedha za kigeni nchini

DAR ES SALAAM-Ripoti ya Uthabiti wa Kifedha Tanzania Disemba 2022 imeonesha kuwa,akiba ya jumla ya fedha za kigeni ilifikia dola za Kimarekani milioni 5,177.2 mwishoni mwa Desemba 2022 ikilinganishwa na dola milioni 6,386.0 mwaka 2021, hasa kutokana na bili za juu za uagizaji bidhaa wakati bei za bidhaa duniani zikiongezeka.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti hiyo ya kila mwaka ambayo huwa inatolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ikiwa imetayarishwa na benki hiyo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha nchini.

Aidha, ripoti hiyo imebainisha kuwa,hifadhi ilitosha kuchukua takribani miezi 4.7 ya makadirio ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, juu ya nchi na viwango vya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) vya miezi 4.0 na miezi 4.5, mtawalia.
Bofya hapa, kupakua ripoti yote

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news