DAR ES SALAAM-Mlinda mlango, Ayoub Lakred (28) raia wa Morocco amejiunga na kikosi cha Klabu ya Simba kutoka FAR Rabat kwa mkataba wa miaka miwili.

Lakred ameiongoza FAR Rabat kushinda ubingwa wa Morocco msimu uliopita na kuifikisha Nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Lakred anakuja kuungana na Ally Salim, Hussein Abeli na Ahmed Feruz kipindi hiki mlinda mlango Aishi Manula akiendelea kuuguza jeraha lake. Uongozi wa simba SC unasema kuwa,unategemea uwezo wa Lakred utaimarisha lango lao kuelekea kuanza msimu mpya wa mashindano.