Bei mpya elelezi za maji,RUWASA Mara yakutana na wadau

NA FRESHA KINASA

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mara imeanza kukutana na watumiaji maji mkoani humo ili kupata maoni yao juu ya bei mpya elekezi za maji.
Ni bei ziliyopendekezwa na Bodi ya RUWASA makao makuu ambazo zitatozwa katika miradi mitano ambayo ni ya majaribio katika kila wilaya hapa nchini. 

Agosti 21, 2023 RUWASA imekutana na watumiani maji na wananchi wa Kijiji cha Sirorisimba na Masurura wilayani Butiama mkoani humo.

Ambapo pia, wananchi hao wameipongeza RUWASA tangu ilipoanza mwaka 2019 huduma ya maji safi na salama imeendelea kuwanufaisha wananchi wanaoishi vijijini. 

Dkt.Noel Komba kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara akisoma bei mpya zilizopendekezwa kwa watumiaji katika Kijiji cha Sirorisimba amesema, kwa wateja wa majumbani uniti moja ni shilingi 1700 kwa uniti.
Wateja wa taasisi Shilingi 2, 000 kwa uniti, wateja wa viwandani Shilingi 2,300 kwa uniti na wateja wa magati Shilingi 2000 kwa uniti. 

Ambapo bei ya zamani amesema ilikuwa Shilingi 2,000 kwa uniti moja kwa wateja wa majumbani, taasisi Shilingi 2000 kwa uniti moja, biashara Shilingi 2,000 kwa uniti moja, viwandani Shilingi 2000 kwa uniti na Vilula Shilingi 2,000 kwa uniti moja na kwamba bei hiyo itadumu kwa miaka mitatu.

Aidha Dkt.Komba amesema, lengo la kuanzishwa kwa RUWASA ni kutatua changamoto ya maji Vijijini na kuendana na dhamira ya Serikali ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kumsogezea huduma ya maji Safi na salama karibu na makazi anayoishi. 

Akizungumza na Wananchi wa Sirorisimba kwa niaba ya Meneja wa RUWASA Wilaya ya Butiama Afisa Maendeleo wa RUWASA kutoka Wilaya ya Butiama, Johnson James Adera amesema kuwa, awali bei ya maji ilipangwa na watumiaji wenyewe.

Lakini bodi ya RUWASA makao makuu imependekeza bei hiyo ili wananchi wazitolee maoni na baraka zao kabla ya kuanza kutozwa.

"Tunao mpango biashara ulioangalia mambo kama ubora wa maji, ushindani wa huduma ya maji, kiwango cha pato la wanufaika na uendeshaji na matengenezo ya mradi. 

"Na lengo ni kutaka kuona mradi inakuwa na uendelevu katika kuwahudumia Wananchi uweze kuwanufaisha wajukuu na vitukuu kwa kudumu muda mrefu.

"Haya yamefanyika kwa hesabu za kitaalamu kabisa na ndio maana tumekuja kuwaambia muweze kutoa baraka zenu tutapeleka mapendekezo yenu RUWASA Dodoma.
"Lakini kwa Sasa bei hizi hazijaanza kutumika. Kwa bei hii mpya ikianza kutumika ndoo ni sawa na Shilingi 34 kwa wateja wa nyumbani,"amesema Johnson. 

Kwa upande wao wananchi wa Sirorisimba kwa idadi kubwa wameyapokea mapendekezo hayo ya bei na kuafikiana nayo kwa uendelevu wa mradi wao. 

"Tangu tumeanza kutumia maji ya RUWASA tunamshukuru Mungu magonjwa ya tumbo yamepungua ambayo awali wananchi tulikuwa tukiugua kama homa ya matumbo, amweba na minyoo, maji haya ni salama,"amesema Asha Daudi Mkazi Sirorisimba. 

Neama Amony Mkazi wa kijiji hicho amesema ,RUWASA wilayani humo na Mkoa wa Mara kwa ujumla imesaidia kuimarisha ndoa, kwani wananchi wanaopata maji baada ya kuvuta majumbani wameondokana na migogoro ya ndoa kwani awali walitembea umbali mrefu na kutumia muda mwingi kutafuta maji. 

Mradi wa maji wa RUWASA katika Kijiji cha Sirorisimba unahudumia zaidi ya Wananchi 3,500, na una bomba lenye ujazo wa lita 100,000. Huku idadi ya Wananchi wa Kijiji hicho wakiwa zaidi ya 4000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news