DAR ES SALAAM-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania na wafanyabiashara nchini kuzipuuza taarifa za upotoshaji ambazo zinasambazwa kwa makusudi katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa, Taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha.
Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache zilizopita baada ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba kubainisha kuwa,wana akiba ya fedha za kigeni, kiasi ambacho kinakidhi uagizaji wa bidhaa na huduma kwa takribani miezi mitano.
Gavana Tutuba aliyasema hayo makao makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam katika mkutano na wafanyabiashara wa maduka ya ubadilishaji fedha za kigeni nchini.
"Natumia fursa hii kuwapongeza kwa mchango wenu katika kutoa huduma za kubadilisha fedha za kigeni kwa wananchi na kusaidia ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi wa nchi yetu kwa ujumla.
"Napenda kuwajulisha kuwa mjadala wa leo ni muhimu kwa maslahi ya biashara zenu, sekta ya fedha na kwa uchumi wa nchi yetu kwa ujumla,"amefafanua Gavana Tutuba.
Katika mkutano huo, wadau hao walipata fursa ya kujadiliana juu ya namna bora zaidi ya kusimamia na kuendesha biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali iliyotolewa na Benki Kuu.
Gavana Tutuba alisema, lengo la kufanya hivyo ni kuongeza ufanisi katika biashara na upatikanaji wa huduma hiyo muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho nchi nyingi duniani zimekumbwa na uhaba wa dola ya Marekani.
"Kama mnavyofahamu, uhaba wa dola ya Marekani umesababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa mahitaji ya dola kutokana na uchumi kufunguka baada ya janga la UVIKO-19, vita kati ya Urusi na Ukraine iliyosababisha kupanda kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo usafirishaji, na hivyo kuongeza mahitaji ya dola."
Pia,Gavana Tutuba alisema, mambo mengine yaliyosababisha uhaba wa dola ni mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyosababisha mahitaji makubwa zaidi ya dola.
Sambamba na sera ya fedha ya Marekani (kupandisha riba) iliyovutia wawekezaji wengi kuwekeza dola zao Marekani na kusababisha uhaba katika mataifa mbalimbali duniani.
"Napenda kuwajulisha kuwa, licha ya changamoto hii ya kidunia, nchi yetu imeendelea kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, kiasi kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kwa miezi isiyopungua minne.
"Mathalani, tarehe 14 Julai 2023, nchi yetu ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni kiasi cha dola za Marekani bilioni 5.55, ambacho kinakidhi uagizaji wa bidhaa na huduma kwa takribani miezi mitano,"alifafanua Gavana Tutuba.
Mbali na hayo, Gavana Tutuba alisema,mafanikio hayo hayawafanyi wabweteke ndiyo maana waliitisha mkutano huo ili wajadiliane namna bora zaidi ya kuwafikishia wananchi huduma ya kubadilisha fedha za kigeni nchini.