NA FRESHA KINASA
KUTOKANA na juhudi kubwa za kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara zinazofanywa na Mbunge wa jimbo hilo, Prof.Sospeter Muhongo zimetambuliwa kwa dhati na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara na hivyo kumpa tuzo ya heshima.
Mbunge huyo amepewa tuzo hiyo kwa utendaji wake wa kazi makini unaogusa maendeleo ya wananchi na utekelezaji wa Ilani ya chama kikamilifu.

Prof. Muhongo amekabidhiwa tuzo hiyo ya heshima na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Patrick Chandi kutokana na umahiri wake, upendo, na uwajibikaji madhubuti katika kuwatumikia wananchi kwa kugusa nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu na sekta nyingine jimboni humo.
Chandi amesema kuwa, Prof.Muhongo amekuwa kielelezo bora katika kuwatumikia wananchi na kukipa heshima Chama Cha Mapinduzi na hivyo amewataka wasomi mbalimbali mkoani Mara kuiga mfano wa mbunge huyo na kuisaidia jamii na chama kwa ujumla katika kufikisha maendeleo kwa wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma Vijijini, Denis Ekwabi amesema kuwa, Prof. Muhongo ameendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa ufanisi mkubwa jimboni humo kwa kufuatilia miradi mbalimbali inayotekelezwa na wakati mwingine kujitoa kuwezesha miradi mbalimbali itekelezeke inayogusa maisha ya wananchi wa Musoma Vijijini.
Kwa upande wake Prof.Muhongo ameshukuru na kusema kuwa, ataendelea kuwatumikia wananchi wa Musoma Vijijini kwa moyo wa dhati ikiwemo kuwapa ushirikiano, kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi akishirikiana na Serikali na Chama Cha Mapinduzi na kushiriki katika agenda nzima ya maendeleo kwa pamoja na wananchi jimboni humo.
Shabani Bwire ambaye ni mkazi wa Nyakatende Wilaya ya Musoma Vijijini akizungumza na DIRAMAKINI kufuatia hatua hiyo, amekipongeza Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma Vijijini kupitia Mwenyekiti wake, Denis Ekwabi kwa kutoa tuzo hiyo kwa Prof.Muhongo kwani anastahili kwa mambo makubwa ambayo amekuwa akiyafanya jimboni humo.
"Tunashirikiana na Prof. Muhongo vizuri sana, amekuwa akitupa hamasa wananchi kuiunga mkono Serikali kwa yale inayotufanyia na pia yeye kuchangia fedha zake mbali na mfuko wa jimbo kuwezesha miradi.
"Na pia kufuatilia miradi katika kila kijiji, kitongoji na kata kuona kama inakidhi ubora. Chama kimefanya jambo zuri sana kwa kutambua kazi na mchango wa Prof. Muhongo,"amesema Bwire.