Emmerson Mnangagwa (Mamba) arejea Ikulu

HARARE-Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa (Mamba) amechaguliwa kwa muhula wa pili baada ya ushindi wa asilimia 52.6 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi mkuu.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa (katikati) alipowasili kuapishwa jijini Harare mnamo Agosti 26, 2018. (Picha na Jekesai Njikizana, AFP).

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe (ZEC) wakati Mnangagwa akipata asilimia hizo mpinzani wake Nelson Chamisa alipata asilimia 44 wa
Citizens Coalition for Change is a Zimbabwean.

"Mnangagwa Emmerson Dambudzo wa Chama cha ZANU-PF ametangazwa kuwa rais aliyechaguliwa kihalali wa Jamhuri ya Zimbabwe,"Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Chigumba aliwaambia waandishi wa habari.

Uchaguzi huo ulikumbwa na ucheleweshaji uliochochea shutuma za upinzani za wizi na ukandamizaji wa wapiga kura, lakini kundi dogo la wafuasi wa chama tawala walisherehekea matokeo siku ya Jumamosi.

Aidha, upinzani umedai kwamba kumekua na udanganyifu mkubwa na waangalizi wa Kimataifa wanasema uchaguzi huo haukukidhi viwango stahiki vya kidemokrasia.

Mnangagwa, ambaye alichukua wadhifa wa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe baada ya mapinduzi ya jeshi mwaka 2017, alitarajiwa kuchaguliwa tena licha ya kuendelea kwa msukosuko wa kiuchumi nchini humo.

Wachambuzi wanasema kuwa, mchuano huo uliegemea upande wa chama cha ZANU-PF. Mugabe alitawala nchi hiyo tangu uhuru na mwisho wa utawala wa wazungu wachache mwaka 1980.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news