Furahika Education College wanaomuunga mkono Rais Dkt.Samia waachilia fursa tena

DAR ES SALAAM-Chuo cha Maendeleo ya Ujuzi, Ufundi na Viwanda (Furahika Education College) kilichopo Buguruni Malapa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam kimeendelea kuwafikia Watanzania popote walipo ndani na nje ya nchi kupitia maboresho mapya ya mfumo wao.Kujiunga na chuo bonyeza hapa

Mkuu wa chuo hicho, David Msuya amesema, "Chuo cha Furahika Education College kwa sasa kimejipanga katika kukuwezesha wewe mwanafunzi kufanikiwa na kuongeza nguvu kazi katika jamii.

"Hapa Furahika tunatoa mafunzo darasani na kupitia mtandao, njia hii itakuwezesha kujifunza kutokea eneo lolote ulipo na utajipatia cheti baada ya kuhitimu. Ni rahisi na popote." 
 
Amesema, chuo hicho ni kati ya taasisi chache za elimu nchini zinazounga mkono kwa vitendo juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuwapatia Watanzania elimu ujuzi ambayo imekuwa na matokeo chanya katika maisha yao.

Miongoni mwa masomo muhimu ambayo yatamuwezesha mwanafunzi kutimiza ndoto zake baada ya kuhitimu chuoni hapo ni uchoraji wa ramani za nyumba ambapo wakufunzi mbalimbali wabobezi watamfundisha mwanafunzi namna ya kubobea katika eneo hili lenye fursa lukuki nchini.

Pia, mwanafunzi ataweza kujifunza ufundi umeme ambapo chuo kupitia wakufunzi wake mahiri kinatoa mafunzo hayo yatakayomuwezesha mwanafunzi kujifunza kuhusu ufundi umeme wa majumbani na umeme wa magari.

Nyingine ni kompyuta ambapo wanafunzi watapata fursa ya kujifunza programu mbalimbali za kompyuta na baada ya masomo watakuwa na uelewa wa kutosha kwa ajili ya kwenda kutumia maarifa hayo katika ajira au kujiajiri wenyewe popote walipo nchini.

Nyingine ni udereva wa magari ambapo kila mwanafuzi atapata nafasi ya kujifunza udereva wa magari aina zote na vyombo mbalimbali vya moto. 
 
Aidha, ukiingia katika mfumo wa masomo online ya mwaka 2023/2024 utakutana na kozi za engineering wa majengo, human resource, cleaning and forwarding,hotel management, tourism and travel, computer ICT, computer application, kilimo na ufugaji, mafunzo ya huduma ndani ya ndege. Nyingine ni mapambo,ususi, make up,ushonaji umeme wa viwandan,ualimu wa chekechea, engineering na nyinginezo ambapo ni wnye ufaulu wa four kuanzia 30 na hata darasa la saba.Kozi zaidi bonyeza hapa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news