Gavana Tutuba afafanua kuhusu fedha za kigeni nchini

NA DIRAMAKINI

"Ninaamini wengine huko mnafahamu kwamba, kuna uhaba wa fedha za kigeni. Lakini, chimbuko la uhaba huu lina maeneo mbalimbali.

UVIKO-19/Vita

"Siku za nyuma tulifafanua kwamba linatokana kwanza na baada ya changamoto ya UVIKO-19 ambayo imepelekea watu waliokuwa karantini walivyokuja kuanza shughuli zao za kiuchumi, wengi wakahitaji fedha za kigeni ili waagize bidhaa zao kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.

"Kwa hiyo waka-create pressure kwenye biashara au mahitaji ya fedha za kigeni.Lakini ya pili tunasema, imechagizwa na vita vya Ukraine na Urusi,ambavyo sasa baada ya kutokea kwa vita vile,imesababisha supply chain ikaathirika, myororo wa usambazaji na ugawaji wa bidhaa na huduma duniani ukaathirika.

"Baadhi ya huduma na bidhaa zikapanda bei,kwa sababu wasambazaji wakubwa walikuwa ni nchi zile za Urusi na Ukraine, kutokana sasa na kuadimika kwa bidhaa ambako kulisababishwa na vita, imesababisha bidhaa hizo kwenye soko la Dunia zikapanda bei.

"Kwa hiyo, mahitaji ya uagizaji wa bidhaa au ya huduma hata kama ni kwa kiwango kile kile, unahitaji dola nyingi zaidi ili uweze kufanya biashara yako.

"Tunataja dola kwa sababu ndiyo currency inayotumika sana, tunasema karibu asilimia 83 kwenye biashara za Kimataifa, watu wanatumia dola, kwa hiyo hizi currencies nyingine zinakwenda ku-share ile asilimia 17.

Mabadiliko ya tabianchi

"Lakini, wakati huo huo tunafahamu kwamba, kuna changamoto pia ya mabadiliko ya tabianchi, tumeona kwa miaka hii ya karibuni, karibu miaka mitatu, tatizo la mabadiliko ya tabianchi limeongeza mahitaji ya fedha za kigeni kwenye ulimwengu wa biashara au kwenye uchumi wa kidunia.

"Na hii inatokana kwamba, kwa mfano maeneo ambayo yalipata ukame, watu wameathirika kwa sababu ule ukame umewaletea labda uhaba wa chakula.

"Kwa hiyo, watu wanaagiza vyakula ili waweze kujikimu na mahitaji, wakati huo huo wanahitaji fedha nyingi za kigeni.

"Lakini,kwa mfano watu waliopata ukame, labda walikuwa wanazalisha umeme kwa kutumia mfumo wa maji, sasa wanahitaji aidha sola au kuagiza mashine kwa maana ya jenereta pamoja na mafuta yake.

"Kwa hiyo, hiyo nayo ina-create mahitaji makubwa ya fedha za kigeni, tumeona kwa wengine ambao labda wamepata mafuriko, mafuriko yamekuja yakamomonyoa barabara, kama ilikuwa ni ya lami, maana yake watahitaji kuagiza lami ambayo watatumia fedha za kigeni.

"Itawezekana wengine labda baada ya kupata mafuriko wanataka sasa kurejesha mfumo, labda wa huduma, maana yake wataagiza magreda,na wanaweza wakaagiza mahitaji mengine ambayo yanahitaji dola.

"Tunapoongelea suala la mabadiliko ya tabianchi,kuna kitu watu wengi huwa hawakielewi, tunasema baadhi ya magonjwa, vijidudu vile vinakuwa na usugu wa kuhimili zile dawa za awali.

"Kwa sababu, lile joto linavyoongezeka au hali inavyobadilika inafanya magonjwa mengine yanahimili ile hali na mengine hata zile dawa ambazo zilikuwa zinatumika zinakuwa hazina uwezo wa kutibu yale magonjwa.

"Kwa hiyo,kwenye suala la mabadiliko ya tabia ya nchi, tumeona tafiti zinatuonesha kwamba, baadhi ya magonjwa yameibuka, na mengine hayawezi yakaponywa kwa kutumia dawa za awali, kwa hiyo pia hapo tunahitaji kuagiza dawa, vifaa tiba na vitendanishi."

Sera za fedha

"Hayo yote yanaendelea ku-create pressure kwenye mahitaji ya fedha za kigeni. Kwa ujumla, ukiangalia kuna changamoto nyingine ambayo imejitokeza ambayo inasababishwa na sera za fedha kwenye uchumi wa Marekani.

"Tunafahamu wote kwamba, sisi Tanzania hatuchapishi dola, ninaamini ninyi mnafahamu, sisi tunachapisha shilingi yetu ya Tanzania, kwa hiyo ukihitaji fedha nyingine, tofauti na shilingi maana yake lazima uende ukaibadilishe kutoka kwenye shilingi ya Kitanzania ili upate hiyo currency nyingine.

"Sasa, sera za Marekani, kutokana na hizo changamoto za UVIKO-19 baada ya watu kufungiwa ndani wakati ule wa karantini, na kutokana na vita vya Ukraine na Urusi na hata changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ule mfumuko wa bei ulipanda, kuna kipindi ulifika mpaka asilimia nane.

"Lakini, benki kuu mara nyingi unapotaka kupunguza mfumuko wa bei, unatumia arrengements mbalimbali labda ya kutoa zile bondi, tunaita liquidity paper kwa ajili ya kupunguza ukwasi wa fedha zilizoko kwenye mzunguko.

"Lakini, wakati mwingine tunatumia utaratibu wa kawaida,kutoka kwenye taasisi za kifedha tunanunua sasa zile fedha ili kwa kufanya hivyo, uweze kupunguza mfumuko wa bei.

"Ila unapopunguza fedha iliyopo kwenye mzunguko, unafanya ile fedha iadimike, fedha ikiadimika, unaifanya ipande thamani, kwa sababu pia fedha ni bidhaa, zile kanuni za kawaida za kiuchumi za demand and supply.

"Ukifanya supply ya fedha inakuwa limited au una-create scarcity ya fedha, lakini wakati huo kama demand iko juu, utafanya gharama au bei ya ile product yako ambayo sasa itakuwa ni hiyo dola, itapanda.

"Kwa hiyo, kwa kufanya hivyo, maana yake unapunguza mfumuko wa bei, sasa bado hii changamoto bado inaendelea kutokana na hiyo sera."

Juhudi za Serikali

"Ingawa tunafahamu juhudi zilizofanywa na Serikali yetu, chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tumeona uchumi wa Tanzania, nao baada ya kutoka kwenye UVIKO-19 unaendelea kuimarika.

"Tumeona takwimu zinaonesha uchumi wa Tanzania unakuwa kwa asilimia 4.7 maana yake shughuli mbalimbali za kiuchumi, zimeendelea kuongezeka, sasa hizo shughuli ukiangalia kwa ujumla wake zinahitaji fedha za kigeni.

"Kwa sababu, baadhi ya bidhaa hazizalishwi hapa, inabidi tuziagize, sasa haya yote yamesababisha changamoto ya uhaba wa dola na fedha nyingine za kigeni."

Mikakati

"Lakini, kuna mikakati mingi Serikali imeifanya, kwanza kuna moja tunaita Import Substitution Initiative ambayo lengo ni kupuguza mahitaji ya bidhaa ambazo zinaweza kuzalishwa ndani ya nchi, lakini kwa sasa tunaziagiza kutoka nje.

"Sasa, tukipunguza mahitaji ya bidhaa hizo,maana yake zitaendelea kuzalishwa Tanzania, na kama zikizalishwa Tanzania fedha za kigeni zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya kuziagiza kutoka nje, hazitahitajika tena, tunapunguza pressure ya matumizi ya fedha za kigeni kwenye uchumi wa Tanzania.

"Ndiyo maana,kwenye hotuba ile ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha, tulisema tunarejesha ule utaratibu wa Export Guarantee Scheme ambao ile ilikuwa na madirisha mawili, dirisha la kwanza la kusapoti wazalishaji wa ndani.

"Wazalishaji wa kati na wadogo, sasa tumeshakamilisha ule muongozo, tunataka sasa tuanze kutoa hizo sapoti kwa watu ambao wanaweza kuongeza thamani kwenye bidhaa zinazozalishwa ndani.

"Ili zikidhi vigezo na viwango vya Kimataifa zitakapouzwa sokoni, Watanzania wanapozipata kwenye soko la ndani zitakuwa na bei ya kawaida ambayo itashindana na bidhaa zinazotoka nje.

"Na, kwa sababu zitakuwa na ubora unaokidhi mahitaji, maana yake wananchi wa Tanzania wataridhishwa na ule ubora wa bidhaa hizo, hawatahitaji tena kuagiza bidhaa kutoka nje.

"Lakini, kama mlifuatilia viozuri kwenye hotuba ile kuna hii sasa ya Export Promotion ambayo tunaongelea kwenye hii ya Export Guarantee Scheme.

"Lengo tunataka kwamba, tuweke dhamana kwenye bidhaa ambazo kama tutaziongezea thamani au kama kuna kitu tunaweza tukafanya hizo bidhaa zetu zikaweza kushindana na bidhaa nyingine zinazozalishwa nje, ziweze kushindana, ziweze kupata ubora mzuri.

"Ziweze kushindana kwa maana ya bei, kwa sababu katika uzalishaji ukitaka kushinda soka la nje, tunasema bidhaa zako lazima uzalishe pale ambako unajiona una comparative advantage au competative advantage.

"Uzalishe kwa wingi ili unapozipeleke kwenye soko la nje ziweze kushinda soko, kwa sababu nguvu ya soko inaangilia zaidi ubora wa bidhaa,inaangalia pia bei iliyopo sokoni.

"Sasa, hayo yote tukiyafanya, sisi kama Benki Kuu ya Tanzania tumetengeneza hilo dirisha ambalo tunataka tushirikishe mabeki ambayo yatakuwa yanapitia ile miradi, wakijiridhisha kwamba miradi ile inaweza kupata ufadhili, sisi tuta-guarantee kwa asilimia kadhaa.

"Tumetengeneza muongozo, kwenye ule muongozo kuna packages tofautitofauti, kuna nyingine inaweza kuwa asilimia zaidi ya 50 hasa pale ambapo mtu anataka kuagiza kama mashine ili yakija kwa sababu malighafi tayari zipo nchini.

"Tunaamini akipata labda hiyo dhamana kupitia Benki Kuu ambayo sisi tutaitoa kupitia kwenye hizo benki nyingine ili na wao waweze kutoa mkopo labda kwa asilimia 50 na sisi tuki-guarantee kwa asilimia 50, bidhaa zile zinaweza kupatikana kwa haraka.

"Au kama ni mashine, lakini sasa yule mzalishaji akishaizalisha tunaamini anaweza kuiuza aidha ndani au nje kama ataweza kushindana kwenye soko,"amefafanua kwa kina Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news