NA LWAGA MWAMBANDE
MMOJA wa wachambuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo ya kiuchumi, 𝑳𝒖𝒔𝒆𝒌𝒆𝒍𝒐 𝑮𝒆𝒐𝒓𝒈𝒆 wakati fualani kupitia chapisho lake alilolibandika katika mitandao ya kijamii akilipa jina la nguvu ya fedha kwenye ulimwengu wa roho,
Alibainisha kuwa, fedha ni kitu cha thamani kilichokubalika na watu wa jamii husika ili kitumike kubadilishana na bidhaa au huduma.

Picha na NT.
Pia libainisha kuwa, fedha ni kitu chenye nguvu sana kwenye ulimwengu wa roho na wa mwili. Anabainisha kuwa, kwenye mazingira ya kawaida (physically) fedha ni kitu kinachoweza kutembea umbali mkubwa sana kuliko kitu kingine chochote kile.
Ukitaka kuhakiki hili, Lusekelo George kupitia andiko hilo anasema,jaribu kuchukua fedha yoyote uliyonayo hapo mfano shilingi mia tano, au elfu moja, au elfu kumi anza kuifuatilia mzunguko wake tangu ilipo mikononi mwako mpaka yule mtumiaji wa kwanza toka kiwandani.
Anasema,utagundua kwamba imepita kwa watu mbalimbali na maeneo mbalimbali. Vivyo hivyo, kama ambavyo fedha inaweza kuzunguka maeneo mengi katika ulimwengu wa mwili ndivyo hivyo inavyoweza kufika maeneo mengi kwenye ulimwengu wa roho.
Pia, anasema fedha inaweza kufanya mambo mengi katika ulimwengu wa mwili. Mfano fedha inaweza kununua nyumba, chakula, shamba, bidhaa na huduma mbalimbali.
Vivyo hivyo kwenye ulimwengu wa roho fedha inaweza kutumika kununua uhai wa mtu,kesi, magonjwa na nyinginezo.
Anasema, upande wa giza wanaelewa umuhimu wa fedha, hivyo wanaweza kutumia fedha kufanya mambo mengi kiroho. Rejea, Mathayo 27:6-8 [6] Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema,Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni kima cha damu.
[7] Wakafanya shauri, wakavitumia kwa kununua konde la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni. [8]Kwa hiyo konde lile huitwa konde la damu hata leo.
Hivyo vilikua ni vipande 30 vya fedha alivyopewa Yuda kama hongo ili amsaliti Yesu. Yuda alipogundua ametenda dhambi nafsi yake ilimsuta akavirudisha kwa wakuu wa makuhani. Maandiko yanasema alipovirudisha, wakuu wa makuhani wakasema si halali kuviweka kwenye kapu la sadaka.
Waliogopa kuvichanganya na fedha zingine kwa sababu vile vipande vya fedha vilibeba roho ya uovu/mauti/usaliti na uharibifu.
Pia, wakuu wa makuhani walijua kwamba hii fedha imebeba roho ya mauti, hivyo kama wangechanganya na fedha zingine roho ya mauti ingeingia mpaka kwenye zile fedha zingine na kuleta madhara kwa watumiaji ndiyo maana wakatumia kununua eneo la kuzikia wageni.
Hivyo, kama fedha hizo wangezitumia kwenye mambo ya kimaendeleo zingeleta matokeo hasi maana zimebeba roho ya mauti ndani yake. Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anabainisha kuwa, ni kweli pesa ni upofu na yote inatakasa. Endelea;

1.Hii ni nguvu ya pesa, bila macho kupepesa,
Kwa wengine ni fursa, wanakwenda wananasa,
Bila kujali makosa, nani hazitaki pesa?
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
2.Unakwenda unagusa, hata viti kupangusa,
Hapo umekwishanusa, kule itokako pesa,
Umekwishamtikisa, kwako hafanyi makossa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
3.Ni nani atamtosa, wakati anazo pesa,
Ni nani atamgusa, kwamba analeta visa,
Ni zamani hadi sasa, si mwenzio mwenye pesa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
4.Mtu yule mwenye pesa, kumwona unapepesa,
Vile shetani mkosa, awa malaika hasa,
Ni sabuni hiyo pesa, makosa inatakasa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakata.
5.Ni ngazi za juu pesa, usonazo hutagusa,
Ni hekima hiyo pesa, hata pasipo msasa,
Inakubalika pesa, nani hataki anasa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
6.Pesa kwa watu hamasa, haki yote kuitosa,
Inayopendwa ni pesa, kiasi kuzua visa,
Asopesa kumtosa, haihitaji darasa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
7.Amekumbatia pesa, imani ameitosa,
Amekumbatia pesa, hasikiii ukiasas,
Amekumbatia pesa, anazioga anasa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
8.Asawazisha makosa, akishagusishwa pesa,
Anabariki makosa, akishalambishwa pesa,
Apuuzia makosa, akishashibishwa pesa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
9.Jawabu la yote pesa, kama wazigusagusa,
Kama una njaa pesa, macho huwezi pepesa,
Mahitaji yote pesa, hakuna cha kukutesa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
10.Ndizo zatawala pesa, kwenye mambo ya siasa,
Ndizo zasikika pesa, masuala ya kanisa,
Migogoro na mikasa, chanzo kikubwa ni pesa,
Ni kweli pesa upofu, yote inayatakasa.
11.Ole kwa mpenda pesa, Muumba utamkosa,
Kufurahia anasa, kwa maovu kutakasa,
Hapo ulipo ni tisa, kumi jua utanasa,
Huwa ni upofu pesa, yote inapotakasa.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602