DIPLOMA GPA 2.9-2.0 JIUNGENI FOUNDATION PROGRAMU YA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
Kama wewe una Diploma na GPA yako ni 2.9-2.0 jiunge Foundation ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kisha utajiunga Shahada mara utakapohitimu foundation.
Kumbuka, ili uweze kujiunga foundation, wewe mwenye Diploma unapaswa kuwa na Award Verification Number (ANV) inayotolewa na NACTVET. Ikiwa huna AVN huwezi kuchaguliwa kwani sifa zitakuwa hazijatimia.
Tuma maombi yako sasa hivi kupitia www.out.ac.tz ambapo masomo yanatarajiwa kuanza mwezi Novemba 2023 na kukamilika mwezi Juni 2024.
Kama una swali usisite kuandika ujumbe kupitia nambari 0719017254. Au fika tawi la karibu la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania utahudumiwa.
FORM SIX WENYE SIFA ZIFUATAZO JIUNGENI FOUNDATION PROGRAM
Kama wewe ni mhitimu wa Kidato cha Sita umepata DEE, EEE, CSS, EDS, ESS, DSS, EES, EEF, DEF, kwa ufupi, kama huna D mbili kwenye masomo yako lakini una pass moja na subsidiary moja jiunge Foundation Program ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambayo ni programu ya maandalizi ya kujiunga Degree katika vyuo vikuu mbalimbali.
Tuma maombi yako kupitia www.out.ac.tz
Masomo yataanza Novemba 2023 na kukamilika Juni 2024. Tuma maombi yako sasa hivi. Ada ya programu nzima ni 690,000/= ambayo hulipwa kwa awamu.
Kwa maswali niandikie sms kupitia 0719017254 nitakupatia majibu.
WENU
Dkt. Mohamed Maguo
Mhadhiri Mwandamizi na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania