ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amelipongeza Kanisa la Anglikana Tanzania kwa kuendeleza amani, umoja na mshikamano nchini.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewashukuru viongozi wa kanisa hilo kwa mipango yao ya kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii na Serikali ipo tayari kuendeleza ushirikiano na kanisa katika sekta hiyo.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Maimbo Mndolwa amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar. Vilevile Askofu Mndolwa amesema, kanisa linaendelea kumuombea katika uongozi wake.