Kamati ya Bunge yawaita kutoa maoni

DODOMA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepanga kuujadili MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI NA. 2 WA MWAKA 2023 [THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) (NO.2) BILL, 2023].

Katika kutekeleza jukumu hilo, kwa mujibu wa Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023, Kamati itasikiliza na kupokea maoni ya wadau (Public Hearing) siku ya Jumatano tarehe 16 Agosti, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Frank Mfundo, Ghorofa ya 5 Jengo la Utawala, Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 7, 2023 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

Kamati inawaalika wadau wote wenye maoni kuhusu Muswada huo kufika na kuwasilisha maoni yao. Aidha, maoni yanaweza kutumwa kwa njia ya posta au Barua pepe kwa anuani zifuatazo: -
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro
S.L.P. 941,
40490 Tambukareli,
DODOMA.
Baruapepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz
Muswada huo unaweza kupakuliwa katika tovuti ya Bunge,
https://www.parliament.go.tz/bills-list

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news