Maeneo ya kanisa nchini yaendelezwe kuepuka uvamizi-Mhandisi Sanga

DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga amehimiza maeneo ya kanisa nchini kuendelezwa na kulindwa kwa lengo la kuyalinda dhidi ya wavamizi na kuepukana na migogoro ya ardhi kwa siku za baadae. 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga katika Picha ya pamoja na Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Maimbo Mdolwa mara baada ya mazungumzo ya pamoja mapema leo jijini Dodoma.

Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,Maimbo Mdolwa amefika katika Ofisi za Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Mtumba Jijijini Dodoma mapema leo Agosti 25, 2023 kwa ajili mazungumzo yanayohusu maeneo yanayomilkiwa na Kanisa hilo yaliyovamiwa na Wananchi katika sehemu mbalimbali hapa nchini. 

Katika mazungumzo yake na Kiongozi huyo mkubwa wa Kanisa Katibu Mkuu Sanga amesema wamekubaliana kuunda tume ya pamoja itakayopitia baadhi ya maeneo ya kanisa yenye changamoto ya migogoro ya ardhi ili kuyapatia ufumbuzi wa pamoja.

Aidha,Katibu Mkuu Sanga amelitaja eneo la Kanisa hilo liliko Buza Wilayani Temeke kuwa sehemu ya kanisa hilo ambalo mara baada ya kuunda tume hiyo litafanyiwa kazi bila kuyataja maeneo mengine ya kanisa hilo yenye changamoto ya uvamizi kutoka wananchi wanaotaka kukalia eneo hilo bila kufuata taratibu zilizopo. 

Wizara ya Ardhi ndiyo Wizara yenye dhamana ya kushughulikia masuala yote yanayohusia na Ardhi hapa Nchini na imekuwa ikipokea malalamiko ya wananchi wanao kabiliana na changamoto kama izo ikiwemo uvamizi wa ardhi na kujimilikisha maeneo hayo bila kuzingatia taratibu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news