ARUSHA-Kumekuwepo na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Askari wa Jeshi la Uhifadhi kumpiga na kumjeruhi kijana katika Kijiji cha Nainokanoka ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Mnamo tarehe 13 Julai, 2023 tuliona kwenye mitandao ya kijamii taarifa ya kijanahuyo kujeruhiwa na Askari kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Baada ya taarifa hizo, Mamlaka ilikutana na uongozi wa Kijiji na Kata husika wakiongozwa na Mheshimiwa Diwani kwa lengo la kutaka kujua kilichotokea.
Suala hili tulikabidhi Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi na hadi sasa hakuna ushahidi wowote kuwa Askari walihusika na tukio hilo.
Vile vile, mnamo tarehe 15/8/2023 kundi la vijana takriban 200 walivamia waandishi wa habari na watumishi wa Serikali na kuwajeruhi na kuharibu magari ya Shirika.
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi ilichukua hatua ya kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo na kwamba masuala yote yanashughulikiwa na Jeshi la Polisi na si Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kama inavyopotoshwa.
Mamlaka inapenda kujulisha umma kuwa taarifa zote hizo si za kweli, na zinalenga kuchafua Taasisi pamoja na zoezi linaloendelea la kuhamisha wakazi wanaohama kwa hiari.
Tunatoa rai kwa wananchi wote na wadau waliopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itaendelea kushirikiana na jamii katika kuhifadhi na kulinda rasimali za Taifa.