ARUSHA-Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga amewaongoza viongozi, watumishi na taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu katika Mkutano wa Mazingativu unaoendelea jijini Arusha.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akifuatilia uwezeshaji wa Mada Mbalimbali katika Mkutano wa Mazingativu kwa Viongozi, Watumishi na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Bw. Mohamed Ali Ahmed akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Mazingativu kwa Viongozi, Watumishi na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Mazingativu kwa Viongozi, Watumishi na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mwezeshaji Dkt. Chris Mauki akiwasilisha mada katika Mkutano wa Mazingativu unaoendelea mkoani Arusha, kwa Viongozi, Watumishi na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu).
Mkutano huo unalenga katika kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika utendaji wa kazi ikiwa ni pamoja na uratibu wa shughuli za Serikali.