Naibu Spika afungua mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu

Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua kwa niaba ya Spika wa Bunge Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kamati za Jukwaa hilo zinazotarajiwa kufanya vikao kwa nyakati tofauti ni Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Demokrasia na Utawala Bora.Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Jukwaa hilo pamoja na Wajumbe wengine kutoka Mabunge ya Nchi takribani 12 za Maziwa Makuu wanatarajiwa kushiriki katika vikao hivyo.
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Balozi Onyango Kakoba akizumgumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa (kushoto), Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (katikati) na Mheshimiwa Deus Sangu (kulia) wakimsikiliza Naibu wa Spika Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua Mkutano wa Vikao vya Jukwaa hilo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Mhe. Najma Giga (kushoto) na Mhe. Shamsia Mtamba (kulia) wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua Mkutano wa Vikao vya Jukwaa hilo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA BUNGE).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news