NCAA, Polisi waanza msako Ngorongoro

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imetangaza msako dhidi ya watu wote waliohusika katika tukio la kuwajeruhi wanahabari na watumishi wa Serikali.

"Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inapenda kuujulisha umma kuwa timu ya wanahabari pamoja na watumishi wa Serikali, jioni ya leo (Agosti 15,2023) wamejeruhiwa wakiwa katika jukumu la utoaji elimu kwa wananchi waliojitokeza kujiandikisha kuhama kwa hiari katika Kijiji cha Endulen kilichopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.

"Zoezi la utaoji elimu lilipokuwa likiendelea, vijana wa Kimaasai wakiwa na silaha mbalimbali za jadi, waliwavamia, kuwashambulia na kuwajeruhi kwa silaha wanahabari na watumishi wa Serikali hao;

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa Agosti 15,2023 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Joyce Mgaya.

"Wanahabari na watumishi wote waliopata majeraha katika tukio hilo wamefikishwa katika Hospitali ya FAME Medical iliyopo Karatu kwa matibabu ya dharura.

"Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inawasaka wote waliohusika na tukio hili na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Mamlaka imesikitishwa na kitendo hicho mna inatoa pole kwa wote waliojeruhiwa,"amefafanua Mgaya kupitia taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news