NA MUNIR SHEMWETA
WANMM
KAMATI ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii imelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha linatilia mkazo ukusanyaji madeni ya wapangaji katika nyumba zake.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt.Angeline Mabula akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakati wa uwasilishaji taarifa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Agosti 25,2023.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Timetheo Mnzava amesema, pamoja na shirika hilo kujitahidi katika ukusanyaji malimbikizo ya kodi za wapangaji wake, lakini bado linatakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji madeni kutoka kwa wadaiwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii,Timotheo Mnzava akizungumza wakati Kamati yake ikipokea taarifa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa Kikao cha kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jijini Dodoma leo Agosti 25,2023, Mhe.Mnzava amelitaka pia shirika hilo kuweka msisitizo zaidi katika kuzuia kuzalisha madeni badala ya kusubiri mpaka wapangaji kuwa na malimbikizo makubwa ya madeni.
Sehemu ya watendaji wa Wizara wa Wizara ya Ardhi pamoja na wale wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakiwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kupokea taarifa ya NHC jijini Dodoma leo.
Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Malisili na Utalii wametaka kuwepo mikakati madhubuti itakayowaogopesha wapangaji ili waweze kulipa kodi zao kwa wakati.
Vile vile, Kamati hiyo imeonesha kuridhishwa na utendaji kazi wa shirika hilo katika kutekeleza miradi yake ambapo wamelitaka Shirika kuangalia namna ya kujenga nyumba za gharama nafuu kwa kutumia teknolojia rahisi.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah akiwasilisha taarifa ya Shirika lake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii jijini Dodoma leo.
‘’Niipongeze NHC pamoja na Wizara ya Ardhi maana kazi za shirika zinaonekana hata kwa macho ila nisisitize muweke jitihada pia katika ukarabati wa nyumba zenu ili wapangaji wakae vizuri,’’alisema mjumbe wa kamati, Cecilia Paresso.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Lucy Kabyemera akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakati wa uwasilishaji taarifa ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula akizungumza mbele ya Kamati hiyo amesema, kwa sasa upo uhitaji mkubwa wa nyumba na serikali iko katika marekebisho ya sera ili kuwezesha ushiriki wa taasisi na sekta binafsi katika uzalishaji nyumba.