Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussen Omar akioneshwa nakala ya Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya Mwaka 2022 na Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Numpe Mwambenja alipotembelea banda la ofisi hiyo katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa maarufu Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa mifumo Endelevu ya Chakula.”
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt.Hussen Omar akiuliza jambo kwa Afisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma kutoka kwenye Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bi. Rachel Lugoe wakati alipotembelea banda la ofisi hiyo katika Maonesho ya Nane Nane jijini Mbeya.
Mratibu wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Henry Kissinga akitoa maelezo kwa wanafunzi kuhusu masuala ya Afya Moja walipotembelea katika banda la ofisi hiyo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Jijini Mbeya.
Mratibu kutoka Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bi. Mwansiti Omari akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussen Omar alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakati wa maonesho hayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussen Omar (kulia) akioneshwa picha ya muonekano sahihi wa Bendera ya Taifa, anayemuonesha ni Mpigachapa Msaidizi Mwandamizi, Bw.Mrebo Jorwa (kushoto) alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Maonesho ya Nane Nane jijini Mbeya.
Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Mbeya, Bw. Emmanuel Petro akitoa elimu ya masuala ya UKIMWI kwa vijana walioko kwenye mradi wa Dream waliotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakati wa maonesho ya Kilimo ya Kimataifa- Nane Nane tarehe 5 Agosti, 2023 jijini Mbeya.
Mratibu wa UKIMWI mkoa wa Mbeya, Bw. Emmanuel Petro akitoa elimu ya masuala ya UKIMWI kwa vijana walioko kwenye mradi wa Dream waliotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa- Nane Nane tarehe 5 Agosti, 2023 jijini Mbeya.
Afisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma kutoka katika Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bi. Rachel Lugoe akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa maonesho ya Nane Nane jijini Mbeya.
Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Khowe Malegeri akieleza kuhusu shughuli za uratibu wa maafa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt.Hussen Omar alipotembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nane Nane jijini Mbeya.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).