NA GODFREY NNKO
POSTA Mastamkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC),Macrice Daniel Mbodo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imeonesha ushirikiano mkubwa kwa shirika hilo ili liweze kutoa huduma bora kwa Watanzania.
"Katika maisha yote ya Shirika la Posta Tanzania, halijawahi kupewa nguvu na Serikali kwa kiasi kikubwa kama kipindi hiki cha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, hakika tumepiga hatua nzuri na kupewa heshima kubwa Kimataifa."
Shirika la Posta Tanzania lilianzishwa kwa Sheria Na.19 ya mwaka 1993 baada ya kuvunjwa kwa lililokuwa Shirika la Posta na Simu Tanzania na lilianza kazi rasmi Januari Mosi, 1994.
Aidha,Shirika la Posta linamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100, hivyo ni shirika la watanzania kwa asilimia zote 100.
Hayo ameyasema leo Agosti 14,2023 katika kikao kazi baina ya shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Kikao hicho kimefanyikia Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo ni mwendelezo wa vikao vinavyolenga kuyaleta pamoja mashirika na taasisi zinazosimamiwa na ofisi hiyo ili waeleze umma walipotoka,walipo na wanapoelekea.
Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu amekuwa akisisitiza kuwa, kiu yake kubwa ni kuona taasisi na mashirika hayo yanafanya kazi kwa ufanisi na kwa maslahi ya nchi.
"Kutokana na jitihada kubwa za kuifungua nchi yetu zilizofanywa na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na mageuzi yanayoendelea katika sekta ya Posta hapa nchini,
"Tanzania kama nchi kwa mara ya kwanza tangu kuumbwa kwa mbingu na nchi, imefanikiwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa mamlaka zote tatu za maamuzi ya umoja wa posta duniani."
Pia, Posta Mastamkuu amesema,shirika hilo limefanikiwa kupewa fursa ya kuwa mwenyekiti mwenza na nchi ya Uswisi kuongoza kamati muhimu ya Baraza la Utawala ya Huduma za Posta na Biashara Mtandao (Physical and E Commerce committee).
Amesema, kupitia jukumu hilo,Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara Shirika la Posta Tanzania, Bw. Constantine Kasese ameaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza vikao vya kamati hiyo.
Wakati huo huo, Posta Mastamkuu amezitaja mamlaka za maamuzi za Umoja wa Posta Duniani ambazo Tanzania imeaminiwa na kuchaguliwa kuwa mjumbe zikihusisha Mkutano Mkuu (Congress);
Amesema, Mkutano Mkuu (Congress) ndiyo mamlaka ya juu ya maamuzi yote. Mamlaka hii hukutana kila baada ya miaka minne na wajumbe wake ni mawaziri wenye dhamana ya kusimamia Sekta ya Posta katika nchi mwanachama.
"Jukumu kuu la mamlaka hii ni kutengeneza mkakati wa posta zote duniani wa miaka minne, kufanya marekebisho ya katiba, kanuni na kuchagua Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani na Msaidizi wake."
Nyingine ni, Baraza la Utawala (Council of Administration-CA), ambapo Posta Masta Mkuu amesema, Baraza la Utawala (Council of Administration) ni mamlaka inayoundwa na nchi wanachama 41 wanaochaguliwa katika mkutano Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani kila baada ya miaka minne.
Baraza hili amesema, hukutana mara mbili kila mwaka ili kutekeleza maelekezo au maamuzi yaliyotolewa na Mkutano Mkuu yaani Congress.
Vile vile kuna Baraza la Uendeshaji (Postal Operation Council-POC) ambalo ni mamlaka inayoundwa na nchi wananchama 48 wanaochaguliwa katika Mkutano Mkuu wa umoja kila baada ya miaka minne. Mamlaka hii ndiyo husimamia uendeshaji wa kila siku wa posta zote duniani.
Mbali na hayo,Posta Mastamkuu amesema,usafirishaji vipeto, vifurushi na mizigo ndani na nje ya nchi kupitia shirika hilo ni salama zaidi.
Amesema, shirika kwa sasa limewekeza na kuna mitambo ya kisasa na ufuatiliaji wa kidigitali kuhakikisha mizigo inafika salama na kwa haraka zaidi.
Postamasta Mkuu ameendelea kutoa wito kwa wajasiriamali kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya shirika hilo, kwani anaweza kusajili biashara yake bure kwenye duka la mtandaoni la posta (http://stamps.tz.post) na unaweza kuuza bidhaa yako ndani na nje ya nchi kwa urahisi.
Naye Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) amesema kuwa, shirika hilo limepiga hatua kubwa kutokana na jitihada na uwekezaji unaofanywa na serikali.
Pia ameiomba ushirikiano huo kati ya serikali na vyombo vya habari usiishie kwenye mashirika ya umma pekee bali uende hadi ngazi za wizara ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kati ya serikali na wananchi wake.
“Utaratibu huu uendelee si tu kwa mashirika ya umma bali hata wizara, zipo wizara ambazo kwakweli zinafanya mambo makubwa, lakini mawaziri wake wanateleza kuliko kambale, lakini zipo wizara zinafanya mambo ambayo hata hazijui zinafanya nini.
"Nchi nyingi za ulimwengu wa tatu zinachelewa katika maendeleo si kwa sababu hazina rasilimali, si kwa sababu hazina watu wenye ujuzi, ni kwa sababu ya mawasiliano, kwa hiyo tujenge utamaduni wa mawasiliano, tujenge utamaduni wa kuzungumza,"amesisitiza Balile.
Katika hatua nyingine, Posta Mastamkuu amebainisha kuwa,kwa mujibu wa Sehemu ya III, Kifungu cha 8 (1) cha Sheria iliyoanzisha Shirika la Posta Tanzania, shirika limepewa majukumu ya msingi manne ikiwemo kutoa huduma za Posta ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jukumu lingine ni kutosheleza mahitaji ya kitaifa ya huduma za Posta ya Viwanda, Biashara na jamii kwa ujumla ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kutoa huduma za kutuma na kulipa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia njia mbalimbali zitakazoonekana zinafaa.
Sambamba na kutoa huduma za kaunta za shirika na za Serikali kwa wananchi kulingana na malengo yaliyotajwa katika sheria ya uanzishwaji wa shirika.