Prof.Muhongo kukagua miradi, kuchangia maendeleo jimboni

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo anaendelea na ziara za kukagua na kuchangia miradi ya maendeleo jimboni humo kwa manufaa ya wananchi.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Agosti 5, 2023.

Ambapo taarifa hiyo imesema kuwa, wananchi wanapewa muda wa kutosha kueleza kero na matatizo yanayowakabili kwa ufumbuzi.

"Ratiba ya Alhamisi ya Agosti 10,2023 saa 4 asubuhi ziara itaanzia Kitongoji cha Ekungu, Kijiji cha Kigera, Kata ya Nyakatende. Saa 9 alasiri ziara itaendelea Kitongoji cha Kukaranda, Kijiji cha Chimati, Kata ya Makojo katika ujenzi wa shule mpya ya msingi.

Harambee ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji

"Rejea Ratiba za awali Jumatatu ya Agosti 7, 023. Ukaguzi wa Miradi ya Maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria vijijini Bwasi (Kata ya Bwasi) na Mabuimerafuru (Kata ya Musanja).

"Jumatano ya Agosti 9,2023 Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti, Kata ya Suguti. Uzinduzi wa utoaji wa Huduma za Afya kwenye Hospital ya Halmashauri yetu (Musoma DC). Hospitali hiyo ina hadhi ya Hospitali ya Wilaya. Wote mnakaribishwa,"imeeleza taarifa hiyo.

Matha James mkazi wa Suguti amepongeza hatua ya Prof.Muhongo ya kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali jimboni humo na kusikiliza kero za wananchi.

"Prof. Muhongo amekuwa mbele sana kusukuma maendeleo ya jimbo letu la Musoma Vijijini kwa kutoa michango yake ya fedha na vifaa kujenga miradi mbalimbali na pia anatuwakilisha vyema bungeni.

"Kero zetu anazisikiliza na kuzitatua pamoja na kuzifikisha serikalini na ndio maana Serikali imezidi kutoa fedha za miradi mingi ya maendeleo jimboni mwetu,"amesema Matha James.

Naye James Bwire mkazi wa Nyakatende amesema kuwa, hatua ya Prof. Muhongo kuwa karibu na wananchi inaimarisha mahusiano mazuri baina ya wananchi na Serikali.

"Mbunge anasikiliza kero za wananchi na kuzichukua akiwa katika ziara hii inatupa hamasa wananchi kuipenda Serikali yetu. Lakini pia kunaongeza usimamizi madhubuti wa miradi inayotekelezwa kupitia ufuatiliaji anaoufanya kwetu wananchi ni faraja sana tunashirikiana naye ili dhamira yake ya kuleta mageuzi ya kimaendeleo Musoma Vijijini izidi kufanikiwa zaidi,"amesema Bwire.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news