ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi leo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said amebainisha kuwa, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Soud Said Ali kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC).
Aidha, taarifa hiyo imefafanua kuwa, kabla ya uteuzi huo ambao umeanza leo Agosti 30,2023, Soud alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, na Vya Kati (SMIDA).
Ndugu Bakari Haji Bakari aliyekuwa anashika wadhifa huo, kwa mujibu wa taarifa ya Mhandisi Zena atapangiwa kazi nyingine.