Wajumbe wa Kamati ya Mwaka Mpya wa Kiislamu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza Agosti 21,2023 wakati wa hafla ya kuwakabidhi Vyeti Wajumbe wa Kamati hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. (Picha na Ikulu).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi, kuzungumza na Viongozi wa Dini na kukabidhi Vyeti vya Shukrani kwa Wajumbe wa Kamati ya Mwaka Mpya wa Kiislamu,hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti cha Shukrani Bi.Aziza Omar Hemed, kwa kutambua mchango wake wa Ushiriki na Ufanikishaji wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu Zanzibar 1445, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe.Haroun Ali Suleiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimpongeza Sheikh Mohammed Suleiman Ali, baada ya kumkabidhi Cheti cha Shukrani kwa kutambua mchango wake wa Ushiriki na Ufanikishaji wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu Zanzibar 1445, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti cha Shukrani Ustadh Slum Seif Suleiman kwa kutambua mchango wake wa Ushiriki na Ufanikishaji wa Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu Zanzibar 1445, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe.Haroun Ali Suleiman.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Kamati ya Mwaka Mpya wa Kiislamu Zanzibar wakati wa kukabidhi Vyeti vya Shukrani kwa Wajumbe kamati hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.