Rais Dkt.Mwinyi amshukuru Rais Dkt.Samia kuasisi Tamasha la Kizimkazi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kuasisi wazo la kuwa na Tamasha la Kizimkazi.
Dhamira ikiwa ni kuimarisha umoja, mshikamano na kudumisha mila na utamaduni ili kuchochea uzalendo na kuhamasisha shughuli za maendeleo ya wananchi wa Kizimkazi, Wilaya ya Kusini na Mkoa mzima wa Kusini.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Agosti 26,2023 akifungua Tamasha la msimu wa nane la Kizimkazi uwanja wa Kashangae Paje, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema Tamasha la Kizimkazi miaka michache ijayo litakuwa na mchango muhimu wa kuvutia wageni Zanzibar pia linakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kuongeza vivutio vya utalii nchini kupitia matamasha mbalimbali.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi amefurahishwa na ubunifu wa tamasha hilo kwa kulitumia kuhamasisha maendeleo katika sekta ya afya, huduma kwa makundi maalum, miundombinu, biashara, ujasiriamali na kuimarisha elimu Mkoa wa Kusini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news