Rais Dkt.Mwinyi:Huduma za uzazi salama ni kipaumbele cha Serikali


ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, mwaka huu wa fedha Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kuimarisha huduma za uzazi salama Zanzibar ikiwa ni moja ya kipaumbele chake kikubwa.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Agosti 26,2023 katika mbio fupi na yeye mwenyewe kushiriki matembezi ya hiari ya Kampeni ya Uzazi ni Maisha yaliyoanza Kiembe Samaki na kumalizika viwanja vya Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewashukuru Amref Health Africa kwa kutoa msaada wa gari (mobile van) ambalo litakuwa msaada muhimu kwa Wizara ya Afya kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kusafirisha wataalamu.

Sambamba na sampuli na kutoa huduma za upimaji pamoja na ushauri nasaha kwa wananchi katika vituo mbalimbali vya afya Zanzibar.

Vilevile, Rais Dkt.Mwinyi amefurahishwa kusikia kwamba Kampeni ya Uzazi ni Salama ilioandaliwa na Shirika la Amref Health Africa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya itakuwa ya miaka mitatu mfululizo na imeanza tangu mwaka 2022 na itamalizika mwaka 2024.

Lengo ni kukusanya shilingi Bilioni moja kwa madhumuni ya kununulia vifaa tiba katika hospitali kusaidia uzazi salama na kuimarisha afya ya mama na mtoto wakati wa ujauzito kabla na baada ya kujifungua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news