ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Amaan umefikia hatua nzuri ya kuridhisha na kukamilika kwa wakati ifikapo Disemba, mwaka huu.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Amaan.
Aidha , Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa matarajio ya Serikali kuwa sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar za kutimiza miaka 60 Januari mwakani zitafanyika katika uwanja huo.
Vilevile, uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza watu 15,500 pia kutakuwa na viwanja vidogo viwili vya mpira wa miguu.