NA GODFREY NNKO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:
A. Uhamisho wa Naibu Mawaziri
i. Mhe. David Ernest Silinde amehamishwa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Mhe. Alexander Pastory Mnyeti atakuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
B. Uteuzi wa Katibu Mkuu
Amemteua Balozi Mhandisi Aisha Amour kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi.
C. Uteuzi wa Wajumbe wa Wizara ya Mipango
Kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5 (1) (c) cha Sheria ya Tume ya Mipango Na. 1 ya mwaka 2023 amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Tume ya Mipango:
1) Balozi Ombeni Yohana Sefue – Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu
2) Bw. Omar Issa – Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela.
3) Balozi Ami Ramadhan Mpungwe – Balozi Mstaafu na Mjasiriamali.
4) Bi. Maryam Salim – Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Cambodia.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 30,2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.