Rais Dkt.Samia afanya uteuzi Shirika la Reli Tanzania, VETA

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

i) Amemteua Bw. Ally Amani Karavina kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania.

ii) Amemteua Prof. Sifuni Ernest Mchome kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 16,2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus uteuzi huu unaanza mara moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news