DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amemteua Bi. Stella Rwehabuka Kahwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 12, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.
Kwa mujibu wa tarifa hiyo, uteuzi wa Bi.Kahwa ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) umeanza Agosti 6, 2023.