Rais Dkt.Samia ahimiza Watanzania kutunza mazingira

ARUSHA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwahimiza waumini kujihusisha na shughuli za uzalishaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kazi mbalimbali za Kanisa alipotembelea Maonesho Maalum kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023.

Rais Samia amesema hayo leo katika maadhimisho ya miaka 60 ya KKKT yaliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Tumaini, Makumira jijini Arusha.

Aidha, Rais Samia amesema dunia inakabiliwa na changamoto ya usalama wa chakula hivyo ni vyema nchi ikazalisha zaidi kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, ili tuendelee kujitosheleza kwa chakula na tuweze kulisha nchi za jirani na dunia kwa ujumla.

Wakati huo huo, Rais Samia amezitaka taasisi za dini kujiwekea mikakati mahsusi ya kupambana na uharibifu wa mazingira na utunzaji wa mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Vile vile, Rais Samia amesema mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari kama ukame,mafuriko, kutotabirika kwa misimu na hivyo kuathiri kilimo kwa nchi yetu ambayo kwa asilimia kubwa tunategemea kilimo.

Rais Samia pia amesema Serikali imeelekeza jitihada kwenye kuwawezesha wananchi kutumia vyanzo mbadala vya nishati kama sehemu ya mkakati wa kuhifadhi mazingira.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news