Rais Dkt.Samia amjulia hali Jenerali mstaafu Sarakikya,mfahamu kwa kina

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuzungumza na Mkuu wa Majeshi wa kwanza Mstaafu Jenerali Mirisho Sam Hagai Sarakikya wakati alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Mkoaranga Wilaya ya Arumeru Arusha leo Agosti 20, 2023. (Picha na Ikulu).

Hivi karibuni katika moja ya mahojiano yake maalum, Jenerali mstaafu Mirisho Sam Hagai Sarakikya ambaye ni muhitimu wa chuo cha Sandhurst huko Uingereza anaelezea alivyojiunga jeshini mwaka 1959.

Jenerali mstaafu Sarakikya anabainisha kuwa, aliwakuta David Musuguri na Mwita Waitara wakiwa na vyeo vya juu vya nyota ya kitambaa siyo ya chuma mabegani.

Mbali na hayo, Jenerali mstaafu Sarakikya anaeleza kwa undani wa maasi ya mwaka 1964 na utumishi wake jeshini hadi anastaafu jeshi mwaka 2002.

...Kapteni Mirisho Sam Hagai Sarakikya kwa mshtuko mkuu akiwa afisa kijana umri miaka 30 tu mwaka 1964 aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Kwanza,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa Mkuu wa Majeshi nchini.

Ni kufuatia maasi ya Jeshi la KRA mwaka 1964 na Serikali kuamua kuwatimua waasi wote kutoka jeshini kutokana na kukosa uzalendo, hivyo kuanza upya kuunda jeshi litakalokuwa na uzalendo kwa Taifa.

Afisa huyo wa jeshi alipandishwa cheo kuwa Brigedia kwa wakati huo, Brigedia Mirisho Sam Hagai Sarakakya kwa kuwaongoza maafisa wenzake na kwa bahati nzuri hakukuwa na afisa yoyote aliyeshiriki katika maasi hayo yaliyokuja kuzimwa na Jeshi la Uingereza.

Ni jeshi lililoombwa kuzima maasi ya askari, hivyo walishughulika kuunda upya jeshi lililo na mtizamo wa kulitumikia Taifa na wananchi hivyo kuwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Chini ya uongozi wake Jenerali Sarakikya walipewa jukumu la kupatikana jeshi la nchi kavu infanty, jeshi la majini navy, jeshi la anga, na kufuatiwa na kuanzisha pia shule za wapiganaji shule za maofisa, staff college, vyuo vya maofisa. (Ulinzi Channel)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news